Fedha na Siri Matron awaita wote chumbani kufuatilia pesa yake iliyopotea, na fedha zinapatikana kwa Penina. Junior anarudishwa kazini, huku Yusan akinunuliwa na Jambi kumshawishi Kelvin arudiane na Ginia. Jambi anamuua afande anayeichunguza kesi yao. Siri, pesa, uhasama na hila zimeshika moto!